The United Republic of Tanzania

Tanzania Pyrethrum Board

Tanzania Pyrethrum Board

News and Events

WANAWAKE na vijana wameshauriwa kulima zao la pareto

WANAWAKE na vijana wameshauriwa kulima zao la pareto kwa sababu soko lake lipo na bei ni nzuri kwa kuwa kilo moja ya maua yake ni sh 3,500.

Pareto ni zao lililobeba kiua wadudu asili, ambayo inatengeneza dawa mbalimbali za kudhibiti wadudu shambani,kwenye mifugo, ghalani na nyumbani. Mratibu wa zao hilo nchini kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ( TARI), Kituo cha Uyole Mbeya, Billes Nzilano amesema hayo alipozungumza na HabariLeo kuhusu umuhimu wa zao hilo nchini.

Nzilano amesema pareto ya Tanzania imekuwa ikiuzwa katika nchi za Marekani, Kenya, Rwanda na Japan.

“Pamoja na kupeleka huko nje tunataka kuona pareto ikitumika ndani ya nchi kwa kuendelea kutafiti na kuchakata ili kufikia mazao ya mwisho yafike kwenye nchi yetu ili wakulima wafaidi mazao ya pareto na fedha za kigeni pia,” amesema.

Amesema mbali na matumizi hayo ya kiua dudu, inatumika kama kiungo cha kusukumia perfume. Katika hatua nyingine amesema, Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa zao hilo, lakini ni nchi ya kwanza kwa kutoa pareto kwa ubora.

“Nchi ya kwanza kwa uzalishaji ni Australia. Nyingine ni Kenya na Rwanda,” amesema
Ameitaja Mikoa inayolima zao hilo kuwa ni Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Manyara na Arusha, Naye Mkurugenzi wa TARI Uyole, Dk Dennis Tippe amesema kituo hicho ndicho pekee kinachofanya utafiti wa pareto.

Amesema zao hilo linafanyiwa utafiti kwa sababu miaka ya karibuni kumekuwa kukitumiwa dawa ambazo sio rafiki kwa binadam na mazingira.
” Kwa hiyo pareto ni dawa asili katika kuhifadhi mazao hivyo tunafanya utafiti wa pareto na pia tunazalisha mbegu hizi,” amesema.
 
 

  • PrintFriendly
  • WhatsApp

Copyright Tanzania Pyrethrum Board.